Windows

Kocha Simba SC: Kagera Wakitufunga Tunatwaa Ubingwa

KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ameweka wazi kwamba hata akifungwa kwenye mechi yake ya kesho Alhamisi dhidi ya Kagera Sugar bado atatwaa ubingwa wa ligi kwa sababu hiyo ndiyo tageti yake.

 

Simba kesho Alhamisi watakuwa ugenini mkoani Kagera kwa ajili ya kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar iliyo chini ya kocha Mecky Maxime. Hata hivyo Simba imekuwa haina rekodi nzuri kila inapovaana na Kagera kwani hata msimu uliopita iliagukia pua.

 

Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwake matokeo ya mechi hiyo siyo ishu kutokana na kuwaza kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu kwani hata msimu uliopita alipoteza michezo miwili na wakafanikisha malengo yao.

 

“Mechi na Kagera Sugar siyo ishu sana licha ya kwamba tunahitaji pointi tatu kutoka kwao ili tukae sehemu nzuri zaidi kwenye msimamo wa ligi.

 

“Unajua hata msimu uliopita tulipoteza pointi sita kwao lakini kwa sababu tulikuwa tunataka kombe ndiyo maana tukafanikisha malengo yetu, kwa hiyo hata kwenye mechi hii hata tukipoteza bado hatutakuwa tumepoteza kitu kwa sababu ubingwa ndiyo kitu muhimu,” alisema Mbelgiji huyo.

The post Kocha Simba SC: Kagera Wakitufunga Tunatwaa Ubingwa appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments