Windows

Washindi watano wa Faidika na Jero wa Tigo, SportPesa Wapatikana

 

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (katikati) akiongea na wanahabari.

 

WASHINDI watano wa Promosheni ya FAIDIKA na JERO inayoendeleshwa na Kampuni ya Tigo Tanzania na SportPesa Tanzania wametangazwa leo.

Prmosheni hiyo ilizinduliwa wiki iliyopita ambayo kwa inawahusisha wateja wa TigoPesa pekee wanapocheza na SportPesa.

Katika promosheni hiyo mshindi wa kwanza aliyeshinda ni Franky Victor Kimambo kutoka Kimara Temboni jijini Dar es Salaam aliyejishindia simu ya smartphone.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema hiyo ndiyo droo yao ya kwanza kuchezeshwa tangu promosheni hiyo ilipozinduliwa.

Tarimba alisema kuwa kila wiki wataendelea kutoa washindi watano watakaocheza na SportPesa na washindi hao waliopatikana wa wiki iliyopita mara baada ya uzinduzi huo kufanyika.

Aliongeza kuwa simu hizo smartphone zitatolewa kwa washindi wadogowadogo kabla ya hile kubwa ya gari mpya aina ya Renault Kwid kwa kubashiri kuanzia kiasi cha Shilingi 500 tu ambayo itatolewa mwezi ujao.

“Kwa jero kabisa mtu anajishidia zawadi ya gari jipya aina ya Renault Kwid ambalo ni zilo kilomita lisilowahi kutumika pale unapocheza na SportPesa kupitia TigoPesa.

” Ni baada ya kucheza na SportPesa kupitia TigoPesa pekee kupitia promosheni yetu ya FAIDIKA na JERO.

“Hii ni promosheni yetu ya pili kuchezesha SportPesa tulianza kwa kutoa bajaji 220 na safari hii tunatoa gari jipya kabisa lenye zilo kilomita, ” alisema Tarimba.

Kwa upande wa Kunda Ngoi ambaye ni Mtaalamu wa Huduma za Kidigitali kutoka Tigo alisema kuwa “Ni muda muafaka kwa Watanzani kufanikiwa kwa kupata ushindi wa gari jipya lenye zilo kilomita na simu za smartphone ambazo hizo zitatolewa kwa washindi watano watakaopatikana kwa kila wiki.

The post Washindi watano wa Faidika na Jero wa Tigo, SportPesa Wapatikana appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments