Windows

Canada yachukua takataka zake kutoka Ufilipino

Tani kadhaa za takataka za Canada ambazo ziliachwa nchini Ufilipino kwa miaka kadhaa, hatimaye zimerudishwa Canada jana.

Hivyo kumaliza mzozo wa kidiplomasia ambao ulionyesha namna ambavyo nchi za bara Asia zimechoshwa kutumiwa kama eneo la kutupia takataka.

Mwandishi wa habari wa shirika la AFP aliyeko Vancouver amesema meli iliyobeba makonteina 69 ya takataka, ilitia nanga katika bandari iliyoko viunga vya Vancouver.

Maafisa wa Canada wamesema takataka hizo zitapelekwa katika kiwanda kinachobadilisha takataka kuwa nishati.

Mzozo kuhusu takataka hizo ulianza kati ya mwaka 2013 na 2014 wakati kampuni ya Canada ilisafirisha shehena ya takataka kwa kudanganya kuwa zilikuwa plastiki kutumiwa na Ufilipino.

Post a Comment

0 Comments