Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inaendelea kujifua uwanja wa Taifa yakiwa ni maandalizi kuelekea michuano ya AFCON 2019 inayoanza Juni 21 nchini Misri
Nyota aliyemaliza mkataba katika kikosi cha Yanga Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji wanaojifua wakiwania nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha kocha Emmanuel Amunike kitakachoelekea Misri
Kelvin Yondani, Feisal Salum na Gadiel Michael ni nyota wengine wa Yanga ambao wako katika kikosi hicho
Stars inatarajiwa kuondoka nchini Juni 07 kuelekea Misri
0 Comments