MLINDA mlango wa Yanga Ranadhani Kabwili amesema bado hawajafikia muafaka na mabosi wa timu moja nchini Sudan.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kabwili alisema; “Mkataba wangu na Yanga umekwisha na bado sijaongeza mkataba mwingine, kwa sasa naendelea na mipango yangu mingine ikiwa ni pamoja na kuangalia ofa ambazo nipo nazo mkononi.”
“Kuna timu moja ipo nchini Sudan ambayo inahitaji huduma yangu wakati ukifika nitaweka wazi kila kitu.
“Kipaumbele changu cha kwanza ni timu yangu ya Yanga ofa yao lazima niifanyie kazi ukizingatia wao ndiyo wamenilea na kunifikisha hapa nilipo, ni suala la wakati,” alisema Kabwili.
The post Kabwili kutimkia Sudan appeared first on Global Publishers.
0 Comments