Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla ameshinda nafasi ya Ujumbe wa uwakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Bodi ya Ligi kwenye uchaguzi uliofanyika leo kwenye mkutano wa sita wa Bodi ya Ligi.
Msolla alishinda kwa kura 14 za ndio na 4 hapana huku Herry Nassor akishinda kwa kura 16 na mbili hapana.
Katika nafasi hiyo iliyokuwa inahitaji watu watatu walijitokeza wawili ambapo Dk Msolla alikuwa na Herry Nassor ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya KMC na kura hizi zilipigwa kwa wajumbe wa Ligi Kuu tu.
Kwa upande wa wawakilishi wa klabu za Ligi Daraja la kwanza walijitokeza watatu huku wakihitajika wawili, Brown Ernest (Mwenyekiti Mbeya Kwanza) alishinda kwa kura 34 za ndio na 10 hapana, Juma Lupangilo alishika nafasi ya pili (Mwenyekiti wa Ihefu)alipata kura za ndio 25 huku hapana zikiwa 17 na wa mwisho akiwa Abdul Mohamed (Mwenyekiti African Lyon) akiwa na kura 14 za ndio na 27 za hapana.
Abdul Mohamed awali aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu ya Azam Fc kabla ya kuondoka katika nafasi hiyo.
Kwa upande wa Ligi daraja la pili, Azim Khna (Mwenyekiti Dar City) ambaye alikuwa mwenyewe alipata kura 40 za ndio na moja hapana.
Kura za Fdl na Sdl zilipigwa na wajumbe wote waliokuwepo katika mkutano huku kura za Ligi Kuu zikipigwa na wawakilishi wa Ligi Kuu pekee.
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANANI kutoka Play Store.
0 Comments