Uongozi wa klabu ya Yanga utatoa taarifa rasmi juu ya tetesi zinazowahusu wachezaji wanaodaiwa kuomba kuvunja mikataba yao kutokana na madai ya mishahara
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema masuala hayo ambayo yameibuliwa leo watayajibu Jumanne
"Jana tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu kufuatia msiba wa mchezaji wetu wa zamani Ally Yusuf Tigana. Pia tuliwapa ruhusa wachezaji wa kigeni ambao walihitaji kusafiri kwenda kuziona familia zao," amesema
"Lakini leo tumeamka asubuhi tukakutana na taarifa zinazohusu wachezaji kuvunja mikataba kwenye mitandao ya kijamii. Hivyo tuvute subira muda sio mrefu tutaweka hadharani taarifa sahihi kujibu hayo yanayozungumzwa. Hatuwezi kuyazungumza leo kwa sababu mengine ni ya kiofisi, ni vyema tusubiri siku ya kazi"
Wakati Bumbuli akiyazungumza hayo, taarifa za uhakika ni kuwa mshambuliaji Sadney Urikhob yeye huenda asirejee baada ya mkataba wake kuvunjwa
Sadney aliomba mkataba wake uvunjwe na uongozi wa Yanga ulikubali ombi lake baada ya kushauriana na Kamati ya Ufundi
Hakuna gharama ambazo Yanga itaingia baada ya uamuzi huo
Sadney ameifungia Yanga mabao mawili tu, tangu alipotua mwanzoni mwa msimu
Alifunga bao kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC
Aidha taarifa za beki Lamine Moro kuandika barua kuomba mkataba wake uvunjwe pia ni kweli.
Pengine uongozi wa Yanga utafafanua kile kilichoelezwa na beki huyo kupitia barua yake kuwa anadai mshahara wa miezi mitatu
Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Jangwani kutoka Play Store.
0 Comments