Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewaonya watu wanaotumia matusi na kuongeza kuwa ni watu waliokosa malezi kwa namna tofauti tangu wakiwa wadogo hivyo kuitaka Jamii ya Watanzania kutumia nguvu nyingi katika malezi ya watoto kwa lengo la kuepukana na athari za ukosefu wa malezi ukubwani.
Makamu wa Rais amesema hayo jana jijini Dodoma katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko na zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa wataalam wa maendeleo ya Jamii leo, Jumanne Jijini Dodoma.
Aidha Makamu wa Rais amekemea wanaume wanaotumia lugha za matusi katika maeneo ya masoko kuwa yanasabababisha wakina mama wafanyabiashara sokoni kukosa uhuru na hata kushindwa kuleta watoto sokoni kwaajili ya kuwasaidia kwa kutopenda vijana wao kusikia lugha zisizokuwa na maadili.
“Mnawazalilisha wanawake kwa kuwatukana matusi kwa kutumia viungo vyao, kuwashika au kuwapapasa bila idhini yao kwanini nyie wanaume msishikane wenyewe, vitendo vya kuwazalilisha wanawake havikubaliki kabisa,’’ alisisitiza Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
0 Comments