Windows

Watu 21 wafa kwa mlipuko wa Bomba la mafuta


Inaripotiwa kuwa Watu 21 wameuawa na wengine zaidi ya 71 kujeruhiwa vibaya baada ya bomba la mafuta kulipuka na kushika moto nchini Mexico.

Mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaoaminika kuwa ni wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan.

Wengi waliofariki walikua waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuzuka. Hata hivyo Shirika la mafuta la Pemex limesema moto huo ulitokana na mabomba yaliyowekwa kwa njia ambayo ipo nje ya utaratibu unaotambulika.



from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments