Windows

Stars kujipima na Misri leo



Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, wenyeji wa michuano ya AFCON 2019 inayoanza wiki ijayo


Kuelekea mchezo huo, kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amesema mchezo dhidi ya Misri ni kipimo cha kwanza kwa Stars ambayo itaanza kwa kuchuana na Senegal Juni 23

Amunike amesema atautumia mchezo huo kuboresha kikosi chake kabla ya kuivaa Senegal wiki ijayo

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki

Jana Amunike aliweka hadharani majina ya nyota wake 23 ambapo wataiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo ambayo Tanzania inashiriki kwa mara ya pili baada ya kusubiri kwa miaka 39

Post a Comment

0 Comments