TANZIA: MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP Tanzania, Reginald Mengi amefariki Dunia, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo alivyokuwa anavimiliki ikiwa ni pamoja na ITV.
Mengi alikuwa ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania, amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa Dubai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema kuwa amesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee Mengi kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika:-
"Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo kwenye kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyakazi," ameandika Magufuli.
Mengi pia alikuwa ni Mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys na mdau wa Michezo Tanzania na Afrika Mashariki.

0 Comments