Windows

TANZANIA PRISONS: TUNAISIMAMISHA YANGA KIBABE

BEKI Kisiki wa timu ya Tanzania Prison, Salum Kimenya amesema kuwa mkakati wao ni kuona wanashinda mchezo wao unaofuata dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Mei 2.

Kimenya amekuwa akitimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Prisons ambapo mpaka sasa kwa upande wa mabeki yeye ni namba moja kwa kutupia nyavuni akiwa amefanya hivyo mara saba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa tayari kikosi chao kimetia kambi Dar kwa ajili ya kuzoea mazingira na kujiandaa na mchezo wao muhimu kwao.

"Tumejipanga na tupo hapa kwa muda mrefu kujiandaa kuikabili Yanga, nina imani kwa maandalizi ambayo tunayoyafanya tutapata matokeo na hatuna mashaka yoyote.

"Ushindani kwa sasa ni mkubwa nasi tunapambana ili kuona msimu ujao tunaoendelea kubaki kwenye ligi hizo ndizo hesabu zetu kwa sasa mashabiki watupe sapoti," amesema Kimenya.

Yanga wanakumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine, walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.


Post a Comment

0 Comments