Windows

KIPIGO CHA SERENGETI BOYS CHAMKASIRISHA RAIS MAGUFULI, AIPA TAHADHARI TAIFA STARS



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kuwa ameboreka na kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys kufungwa mabao mengi katika ardhi ya nyumbani.

Akizungumza leo wakati wa hotuba mbele ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wilayani Kyela ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi, Magufuli amesema hajafurahishwa na timu ya vijana kufungwa mabao mengi uwanja wa nyumbani.

"Mashindano tumeaandaa wenyewe, uwanja wa kwetu wenyewe, tumefungwa mabao mengi kwelikweli, hili ni jambo la ajabu, tupo watu zaidi ya milioni tano na utashangaa tumefungwa na timu ambayo ina watu chini ya milioni 5, bora ungechukua timu ya Kyela naamini isingefungwa.

"Sasa hili linapaswa liangaliwe kwa usawa, ninatamani siku moja niwe Waziri wa Michezo na nikiwa Waziri wa Michezo timu nitaipanga mwenyewe, kwa hili la kupigwapigwa kwa timu yetu ya Taifa mnaniboa kweli na sijui timu ya wakubwa nayo itakwenda kufungwa? ila sio mbaya huenda kufungwa fungwa nako ni vizuri," amesema Magufuli.

Michuano ya Afcon ambayo imemalizika wikiendi hii, Cameroon imebebwa ubingwa kwa vijana, huku Tanzania ikitolewa na zigo la mabao 12 ya kufungwa na imefunga mabao sita pekee kwenye michezo mitatu.


Post a Comment

0 Comments