LEO Droo ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imefanyika ambapo timu nane zilizotinga hatua ya nane bora zimetambua zitacheza na nani hatua ya robo fainali.
Katika Droo hiyo ukitazama kimahesabu ni wazi inawapa nafasi nzuri Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu soka Tanzania Bara timu ya Yanga kutokana na aina ya timu ambazo anakutana nazo.
Timu hizo ambazo zilitinga hatua hiyo ni pamoja na Yanga, Alliance FC, African Lyon, Azam FC, Lipuli, KMC na Kagera Sugar.
Michuano hii inatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi itakuwa namna hii:-
Yanga wataifuata Alliance ya Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Kagera Sugar wataikaribisha Azam Uwanja wa Kaitaba.
KMC wataikaribisha African Lyon Uwanja wa Uhuru.
Lipuli wataikaribisha Singida United Uwanja wa Samora.
0 Comments