WAKATI Simba ikiwa na spidi kali katika Ligi Kuu Bara hivi sasa, imebainika kuwa endapo itaridhika kidogo tu kidogo basi itakuwa kwenye hatari ya kupoteza mechi zake hasa za mkoani na Pointi 36 huenda zitaipa ubingwa Yanga.
Hivi sasa kuna ushindani mkali kati ya Simba iliyopo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 na Yanga inayoongoza na pointi 64. Yanga imecheza mechi 26 na Simba 20. Yanga imeiacha Simba kwa michezo sita.
Kwa kawaida, timu hizo zimekuwa na matokeo ya kubahatisha zinapocheza mikoani, na kwa mechi zilizosalia ili kumaliza msimu huu, Simba imebakiwa na michezo nane mkoani na Yanga minne. Yanga mechi zake hizo ni sawa na pointi 12 na zile za Simba ni sawa na pointi 24.
Kwa kiasi kikubwa, Yanga tayari wametua mzigo kwa michezo yao ya mikoani ambapo wamesaliwa na mechi dhidi ya Lipuli FC, Ndanda FC, Biashara United, Mtibwa Sugar. Katika mechi ambazo Yanga imecheza mkoani na matokeo yake ni Mbao FC (0-1), Alliance (0-1), Coastal Union (1-1), Mwadui (1-2), Mbeya City (1-2), Prisons (1-3), Stand United (1-0), JKT Tanzania (0-1), Kagera Sugar (1-2), Singida United (0-0) na African Lyon (0-1).
Mechi za mkoani ambazo Simba imesaliwa nazo ni dhidi ya Alliance, Coastal Union, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Prisons, Biashara FC, Singida United na Kagera Sugar. Simba mkoani imecheza dhidi ya Stand United (0-2), Lipuli (1-3), Mbao (1-0), Ndanda (0-0), JKT (0-2) na African Lyon (1-3).
0 Comments