KUTOKANA na mchezaji wa timu ya Alliance FC, Juma Nyangi kuonekana akifanya kitendo kisicho cha kinidhamu kwa mchezaji wa tImu ya Yanga, Gadiel Michael kamati ya nidhamu imeamua kumpa adhabu ili kuwa funzo kwake.
kitendo cha Nyangi kumpapasa makalio mchezaji wa Yanga kilinaswa na kamera za Azam TV kwenye mchezo huo ambao ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu wa klabu ya Alliance, Yusufu Budodi amesema kamati iliamua kufanya kikao kumjadili mchezaji huyo na walimpa nafasi ya kujitetea kabla ya kutoa maamuzi.
"Tumemsikiliza mchezaji wetu na tukapitia kanununi, tukafanya maamuzi ya kumpa adhabu ambayo itakuwa ni funzo kwa wengine ambapo kamati imeamua kumkata mshahara wa mwezi mmoja na kumpa onyo kali.
"Tunaamini itakuwa funzo kwake na tunaomba radhi kwa wadau wa mpira kutokana na kosa la mchezaji wetu, tumeanza kufanya hivyo na hatukuamua kumfungia mechi baada ya kuona ni kosa lake la kwanza," amesema Budodi.
0 Comments