Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe huenda akarejea kunako timu hiyo kwa mkataba wa muda mfupi
Tambwe kinara wa mabao wa muda wote kwa wachezaji wa kigeni ligi kuu ya Tanzania, anaweza kurejea kuitumikia Yanga mpaka mwishoni mwa msimu
Yanga inahitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuachana na washambuliaji Sadney Urikhob na Juma Balinya
Wachezaji hao walishindwa kutamba licha ya matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki
Msimu uliopita Tambwe aliifungia Yanga mabao nane licha ya kutopata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara
Hakuna shaka anaweza kuongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inamtegemea David Molinga pekee
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments