Kindoki aliokoa penalti mbili kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Alliance FC uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba hali iliyofanya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 ambapo itakutana na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Samora mwezi huu.
"Hatua nzuri ambayo nimefikia kwa sasa, ninamshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na uvumilivu hasa katika kipindi kigumu ambacho nimepitia ila yote ni kheri kwangu kwani ni furaha kubwa sana hapa Yanga.
"Mashabiki ni watu muhimu kwangu nawashukuru kwa sapoti yao na kunipa muda wa kufanya mengi zaidi, ninawaahidi kufanya mengi makubwa wazidi kunipa sapoti," amesema Kindoki.
Kindoki alianza kwa kuruhusu 'hat-trick' mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand United uliochezwa Uwanja wa Taifa licha ya Yanga kushinda kwa mabao 4-3.
0 Comments