Windows

Usajili : Achana na Ajibu Simba waigusa tena pabaya Yanga



Hao Simba unaambiwa mipango yao siyo ya kuchekacheka msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa watakayofanikiwa kushiriki kwani mipango ni motoooo.


Baada ya kuelezwa kuwa wapo katika mipango ya kurudisha majeshi kwa mchezaji wao wa zamani Ibrahim Ajibu ambaye amekuwa na misimu miwili mizuri ndani ya watani wao wa jadi Yanga Ibrahim Ajibu unaambiwa hawataishia hapo kuwaumiza Yanga.

Unaambiwa Simba wako katika mipango mingine ya kuhakikisha wanainasa saini ya Kipa wa Yanga Beno Kakolanya ambaye bado atakuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Yanga msimu utakapomalizika wa ligi.

Hata hivyo msomaji wa Kwata Unit inaelezwa kuwa Beno anataka mkataba wake na Yanga uvunjwe lakini Yanga wamekuwa bado wanavutana na Beno na kitaratibu bado mkataba wake na Yanga uko palepale.

hata hivyo kama mambo yatakaa sawa huenda Beno Kakolanya akawa mchezaji huru hivyo kuwa Rahisi kuweza kujiunga na Simba ambao wanamipango ya kuwa na kikosi imara zaidi msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments