UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo watawafundisha soka Alliance kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho licha ya wapinzani wao hao kuweka kambi nchini Rwanda.
Yanga itamenyana leo na Alliance mchezo wa hatua ya robo fainali, Uwanja wa CCM Kirumba na mshindi atakayeshinda atacheza na Lipuli ambayo imekunja nne kwa sasa baada ya kushinda mbele ya Singida United.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema wanatambua mchezo wao utakwa mgumu na kila mmoja anahitaji matokeo ila wamejipanga kuibuka na ushindi.
"Najua wapinzani wetu waliweka kambi huko Rwanda sijui wapi, ila hilo halituumizi tunachotambua kwamba tunaingia uwanjani kutafuta matokeo.
"Wapinzani wetu wana timu nzuri kwa kuwa tumecheza nao na tunawajua ila kwa sasa tunahitaji kusonga mbele hatua ya nusu fainali mpaka hatua ya mwisho ya mashindano haya," amesema Ten.
0 Comments