Windows

ZAHERA AAHIRISHA MAZOEZI YANGA, WACHEZAJI WAISHUHUDIA SIMBA IKIIMEZA AHLY LIVE




Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kililazimika kuahirisha mazoezi mjini Morogoro ili kungalia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Katika mechi hiyo, Simba imepata ushindi wake wa pili hatua ya makundi kwa kuichapa Ahly kwa bao 1-0 lililofungwa na Meddy Kagere.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kufanya utaratibu huo kama sehemu ya kuwasoma Simba kabla ya mechi yao itakayochezwa Jumamosi mjini Dar es Salaam.

Yanga ipo kambini mjini Morogoro, lakini Zahera aliamua kuahirisha mazoezi na sehemu ya programu yake ikawa ni kuwaangalia Simba.

“Kocha aliamua hiyo iwe sehemu ya programu kwa kuwa baada ya mechi hiyo, Yanga inakutana na Simba,” kilieleza chanzo.

Yanga ipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 23 wakati Simba ya tatu ikiwa na pointi 36 baada ya mechi 15.


Post a Comment

0 Comments