MAPEMA mwaka huu kuliibuka taarifa za mwanaume mmoja ambaye ni rubani wa ndege aitwaye Hamdan Zakwani ‘Danzak’ aliyetangaza kumuoa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye wikiendi iliyopita walinaswa ‘live’ hotelini.
MECHI YA STAR VS UGANDA
Kabla ya kunaswa wakizama hotelini usiku mnene wa Jumapili iliyopita, Amani liliwapiga chabo Wema na Danzak wakijiachia kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda The Cranes ijapokuwa hawakujiachia waziwazi ili watu wasiwaone ila kuna wakati walishuhudiwa wakibadilishana namba za simu. Wawili hao walishuhudiwa wakipagawa na ushindi wa Taifa Stars wa bao 3-0 dhidi ya Uganda katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Baada ya hapo sasa, Amani liliamua kuwafuatilia hatua kwa hatua kujua kinachoendelea kati ya wawili hao kwani umepita muda mrefu bila kujua walifikia wapi kwenye masuala yao ya uchumba.
NDANI YA SERENA
Hata hivyo, nyapianyapia ya gazeti hili ilizaa matokeo baada ya kuwaona wawili hao wakiingia hotelini wakiwa pamoja pale Serena Hotel maeneo ya Posta jijini Dar, huku wakiwa na shangwe kama lote kutokana na ushindi wa Stars. Wakiwa ndani ya Serena Hotel, wawili hao hawakupata chansi ya kujiachia ‘praiveti’ kwani kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakishangilia ushindi wa Stars.
HAOO SEA CLIFF
Baada ya kuona gozigozi, Wema na Danzak waliondoka hotelini hapo ambapo walielekea maeneo ya Hoteli ya Maison Sea Cliff iliyopo Masaki, jijini Dar kisha walijiachia watakavyo.
Pamoja na usiku kuzidi kuwa mnene, lakini shangwe la wawili hao halikukomea hapo kwani safari iliendelea ambapo walikwenda kuhitimisha kwenye hoteli moja iliyopo maeneo ya Msasani jijini Dar. Likiwa hotelini hapo, Amani liliwafotoa picha kisha liliwasikilizia wawili hao watoke, lakini hawakutoka hadi linaanua jamvi eneo hilo.
WEMA ATAFUTWA HEWANI
Kesho yake, yaani Jumatatu wiki hii, Amani lilimtafuta Wema ili kujua ameamkaje kutokana na uchovu wa kushangilia ushindi wa Stars na kilichoendelea kati yake na Danzak, lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Alipotafutwa Danzak na kusimuliwa taarifa zake na Wema hatua kwa hatua tangu Uwanja wa Taifa, Serena, Sea Cliff hadi hotelini hapo, alicheka kisha akajibu kwa kifupi: “Mambo mazuri hayahitaji haraka.”
TUTOKAKO…
Mapema Januari, mwaka huu, baada ya jamaa huyo kuonesha nia ya kumuoa Wema, mama wa mrembo huyo, Mariam Sepetu alimkaribisha kufika nyumbani kwa ajili ya taratibu nyingine. Hata hivyo, hapo katikati ulipita ukimya mrefu hivyo haikujulikana kama Danzak alikwenda kutimiza taratibu za mama Wema kwa ajili ya kumuoa mlimbwende huyo wa Taji la Miss Tanzania mwaka 2006/07.
DANZAK NI NANI?
Ni Mtanzania ambaye kabla ya kwenda masomoni nje ya nchi amewahi kufanya kazi za muziki katika Kundi la TNG Squard lililokuwa likiundwa na wasanii Agustino John ‘Latino Man’ na Malicki Bandawe kutoka jijini Tanga. Inaelezwa kuwa, mbali na kurusha ndege, bado shughuli za kimuziki ziko kwenye damu ya Danzak na kwamba hata alipomaliza masomo ya urubani, alitua Bongo na kutunga na kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Fall In na Kichaa.
0 Comments