Bocco jana alifunga mabao mawili wakati timu yake ikilipa kisasi cha kufungwa na Mbao bao 1-0 mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba huku wao wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 uwanja wa Jamhuri.
"Ni ngumu kupata matokeo kutokana na ushindani uliopo ila kikubwa kinachotubeba ni ushirikiano uliopo yetu wachezaji pamoja na uongozi bila kusahau nguvu ya mashabiki tunawaomba waendelee kutupa sapoti tutaendelea kupambana," amesema Bocco.
Kwenye vinara wa kutupia TPL, Bocco anashika nafasi ya tatu baada ya kufikisha jumla ya mabao 11 huku kinara akiwa ni Salum Aiyee wa Mwadui ambaye ametupia mabao 16.
0 Comments