WAKATI JKT Queens wakiwa ni vinara kwenye ligi ya wanawake Tanzania wamejikusanyia pointi 42 baada ya kucheza michezo 14 na kushinda yote, Evergreen Queens ya Dar es Salaam na Mapinduzi Queens ya Njombe ni kama moto umekata kutokana na kupata taabu kupata matokeo kwenye michezo ambayo wamecheza.
Ligi ya wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League kwa sasa imesimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo inajiaanda na mchezo wa kuwania kwenda kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani, Tokyo, Japan.
Mpaka sasa tayari Evergreen wamecheza michezo 14 na wana pointi tano huku wakishinda mchezo mmoja, sare mbili, wamepoteza 11 wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo.
Mapinduzi Queens wamepoteza michezo 12 wapo nafasi ya 12 wametoa sare michezo miwili na wana pointi mbili kibindoni.
0 Comments