UONGOZI wa Azam FC umeamua kuwapiga pini mapema wachezaji wake saba kwa sasa ambao mikataba yao ilikuwa inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu ili kuendelea kuwatumia kwa ajili ya msimu ujao.
Azam FC ambao ni mabingwa wa Afrika Mashariki na kati mpaka imekuwa ni klabu ya kwanza kufanya hivyo kutokana na jeuri ya fedha iliyonayo pamoja na kuamini uwezo wa wachezaji wao ambao wanaitumikia Azam FC.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa mipango ya klabu ni endelevu kwa ajili ya kuimarisha kikosi na mchakato wao unaendelea kwa wachezaji wao.
"Mpaka sasa tumewaongezea mkataba wachezaji wetu saba ambao tupo nao na wataendelea kuwa mali ya Azam FC, lengo letu ni kuona kila mchezaji anapata nafasi ya kuitumikia klabu kwa manufaa ya timu na Taifa kiujumla.
"Mwantika (David) miaka miwili, Mahundi (Joseph) miaka miwili, Abdalah Kheri miaka 3, Ngoma (Donald) mwaka mmoja, Bruce (Kangwa) miaka mitatu, Mbaraka (Yusuph) mwaka mmoja, Kipagwile (Idd) mwaka mmoja.
0 Comments