MAN United wana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanambakiza kipa wao David De Gea ambapo sasa Klabu ya Paris SaintGermain wamesema wanamhitaji.
Kumekuwa na kazi kubwa kwa United katika misimu kadhaa iliyopita ambapo kipa huyo amekuwa akiwaniwa na Real Madrid, lakini sasa inaweza kukutana na upinzani mkubwa zaidi kwa kuwa PSG nao wamesema wanamhitaji mwishoni mwa msimu.
Klabu hiyo bora ya Ufaransa inataka kumpa kipa huyo mshahara anaoutaka wa pauni 350,000 (zaidi ya Sh bilioni moja) kwa wiki. De Gea amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye timu hiyo na hivyo inatakiwa kuhakikisha kuwa inampa mkataba mpya au kumuacha aondoke.
Taarifa kutoka kwenye gazeti la The Sun, imesema kuwa PSG wanataka kuwapa United pauni milioni 60 (Sh bilioni 180) kwa ajili ya usajili wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 28.
Hivi karibuni ilielezwa kuwa kipa huyo anataka kuondoka kwenye kikosi cha United na anataka kwenda aidha PSG au Real Madrid. Hata hivyo, United pia wanaweza kuwapoteza kiungo wao Ander Herrera na Juan Mata ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.
0 Comments