Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Ally Mchungahela imempitisha Dk Jonas Tiboroha kuendelea na mchakato wake wa kugombea nafasi ya Uenyikti ndani ya klabu ya Yanga.
Awali Tiboroha alisimama kuendelea na kampeni zake za kugombea uenyekiti ndani ya timu hiyo baada ya uchaguzi wa kwanza kusimamishwa na wanachama ambao walifungua kesi katima mahakama mbalimbali.
Akizungumza na waandishi leo, Mchungahela amesema kuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wanaruhusiwa kuendelea kugombea katika uchaguzi mpya wa klabu hiyo ambao sasa utafanyika Mei 5, mwaka huu.
"Wagombea ambao walikuwa na mchakato wa kugombea nafasi katika ule uchaguzi wa awaki wataendelea kama kawaida wakiungana na wagombea wapya ambao wataanza kuchukua fomu kuanzia Aprili 2.
"Uchaguzi mpya wa Yanga sasa utafanyika Mei 5, mwaka huu na kutakua na siku za kuchukua fomu, usahili wa wagombea na mambo mengine," alisema Mchungahela.
0 Comments