Windows

Aussems aipotezea Tp Mazembe


Hakuna ubishi kuwa Simba imekuwa moja ya klabu inayohofiwa ndani na nje ya Tanzania hasa kutokana na matokeo ambayo imekuwa ikiyapata katika ligi kuu Tanzania bara na kwenye michuano ya kimataifa kiasi cha kutinga hatua ya Robo Fainali Klabu bingwa barani Afrika.


Lakini nyuma ya matokeo hayo mazuri ya Simba kumekuwa na kocha ambaye amekuwa akiiongoza Simba katika mapambano hayo kocha Patrick Aussems.

Kocha huyo msomaji wa Kwata Unit baada ya kuiongoza vyema jana Simba ikicheza dhidi ya Mbao Fc na kupata ushindi wa bao 3 kwa 0 aliulizwa kuhusu maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa Jumamosi 6 April 2019.

Kocha huyo alifunguka kuwa kwasasa hawezi kuiwaza TP Mazembe kwani bado anamchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania siku ya jumatano mechi itakayochezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Post a Comment

0 Comments