Windows

MBELGIJI ATOA MAJIBU YA VIFAA VIWILI VILIVYOTUA KWA MAJARIBIO SIMBA


Baada ya kuhusika katika kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mashindano ya SportPesa jana Uwanja wa Taifa, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema wachezaji waliokuja kwa majaribio wanahitaji muda.

Simba imeleta wachezaji wa kigeni wawili ambao ni Lamine Moro kutoka Ghana na Kisimbo Ayibek kutoka Togo kwa ajili ya majaribio.

Baada ya kuwashuhudia wachezaji hao uwanjani jana, Mbelgiji huyo alisema bado wanahitaji zaidi mechi nyingine ili kujua kama wanastahili kuwepo ndani ya kikosi cha Simba au la.

Alieleza kuwa ni mapema kwa sasa kusema zaidi lolote kwani wamecheza mechi moja pekee hivyo wanahitaji kupewa nafasi kwanza.

Simba imetinga kucheza nusu fainali sawa na Mbao ambao wamewaondoa Gor Mahia FC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Kenya.

Post a Comment

0 Comments