Kotecha amesema salaam hizo ni watu wote wa Mwanza kwani walichokifanya Mbao kimeitangaza vema Tanzania na jiji la Mwanza kwa ujumla.
Ameeleza ushindi huo ni chachu ya kukuza mafanikio kisoka katika jiji la Mwanza na akiamini uwezekano wa kuwa na timu zingine kama Mbao utakuwepo.
Katika mechi hiyo, Mbao alifanikiwa kuibuka na ushindi wa matuta 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.
Mbao sasa imungana na Simba kuelekea nusu fainali ambapo timu hizo mbili zitakutana.
0 Comments