Windows

HAWA NDIYO WABABE WA SIMBA AFRIKA


Februari 2, mwaka huu utakuwa mtihani mwingine kwa Mbelgiji Patrick Aussems na Simba yake kwani watalazimika kuwafuata wababe Al Ahly nchini Misri katika muendelezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi hii itakuwa ngumu kwa pande zote mbili lakini ugumu zaidi upo kwa Simba kutokana na aina ya matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi hiyo dhidi ya AS Vita ya kuchapwa mabao 5-0.

Japo kimahesabu mechi hii inaonekana kuwa mbali lakini iko karibu kabisa na kuna baadhi ya vitu ambavyo Simba wenyewe wanatakiwa kuvifahamu na kufahamu ni aina gani ya wapinzani ambao wanaenda kukutana nao. Makala haya yanakuchambulia baadhi ya vitu ambavyo wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Simba wanapaswa kufahamu mapema juu ya Al Ahly.


WABABE WA AFRIKA 

Hili ndilo jambo la msingi ambalo Simba wanatakiwa kulitambua kwamba wanaenda kupambana na timu ya aina gani. Achana kabisa na TP Mazembe, Esperance au Wydad Casablanca hawa wote siyo kitu mbele ya Al Ahly inapokuja ishu ya ubabe wa Afrika.

Waarabu hawa ndiyo ‘Baba wa Afrika’ kwani wamechukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara nyingi zaidi wakiwa na makombe nane kwenye kabati lao huku mara ya mwisho kunyakua taji hilo ni mwaka 2013.

Pia Simba wafahamu mwaka jana ilibaki kidogo tu watwae ubingwa wa tisa kabla ya kupokonywa tonge mdomoni na Esperance ambapo Al Ahly walishinda kwao mabao 3-1 nyumbani kabla ya kupigwa mabao 3-0 wakiwa ugenini na kuifanya Esperance kushinda kwa jumla ya mabao 4-3.

MCHEZAJI GHALI

Kikosi kizima cha Simba kina thamani ya bilioni 1.3 lakini kwa Al Ahly hiyo ni thamani ya mchezaji mmoja tu. Ndiyo ni thamani ya mtu mmoja ambapo Al Ahly walitumia bilioni 11.5 kuipata tu saini ya Hussein El-Shahat ambaye walimng’oa kwenye klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu, Simba ambaye amevuna fedha nyingi wakati anasajili ni Meddie Kagere ambaye alitua kwa Sh mil 120.

MASTAA WAO

Hapa sasa ndiyo utachoka, wakati Simba wenyewe wakiringia kuwa na kina Okwi, Chama na Kagere, staa mkubwa wa Al Ahly ni Ramadan Sobhi anayecheza kwa mkopo kutoka Huddersfi eld Town ya England. 

Pia kuna mastaa wengine kama El Shahat,Warid Azaro, Mohamed El Shenawy ambaye ni kipa wa Taifa la Misri na wengineo.

WABABE WA NYUMBANI

Al Ahly siyo kwamba ni wababe wa Afrika tu bali ubabe wao unaanzia kwao Misri. Wakiwa kwao Al Ahly wamechukua kila aina ya ubingwa ambao wameugombania na hadi sasa washakusanya
mataji 40 ya Ligi ya Misri tu. 

Wakati Al Ahly wakiwa na mataji 40 ya ligi Simba hadi sasa wana makombe 19 ya ligi. Makombe ya Al Ahly mengine ni Kombe Misri (mara 36), Egyptian Super Cup (10), Cairo League (15) na Sultan Hussein Cup mara saba.

WAKALI WA DUNIA

Hii ndiyo rekodi ambaye Simba inaweza kuwashtusha kabisa kwani wengi wao hawaifahamu. Wakati mashabiki wengi hapa nchini wakizitaja B a r c e l o n a , Real Madrid na M a n c h e s t e r United kwamba ndizo klabu zenye mataji mengi duniani lakini ukweli ni kwamba hao wote siyo kitu mbele ya Al Ahly. R e k o d i z i n a w e k a wazi kwamba Waarabu hao wanakimbiza k a t i k a k u n y a k u a m a k o m b e kwani wana mataji 132 waliyoyatwaa kwenye ligi mbalimbali. Wakati wao wakiwa na 132, Barcelona wenyewe wana 93 na Madrid 90.

Mataji hayo ni yale ya Ligi ya Misri (40), Egpty Cup (36), Egyptian Super Cup (10), Cairo League (15) Sultan Hussein Cup (7) na Ligi ya Mabingwa Afrika (8).

Mengine ni Afro-Asian Club Championship (1), CAF Confederation Cup (1), CAF Super Cup (6), African Cup Winners’ Cup (4), Arab Club Champions Cup (1), Arab Cup Winners’ Cup (1) na Arab Super Cup (1).UWANJA WATAKAOCHEZA

Simba wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani wanaenda kucheza kwenye mazingira magumu zaidi waliyokutana DR Congo mbele ya AS Vita kwani Al Ahly wenyewe wanatumia uwanja wa nyumbani kama silaha ya kuwamaliza wapinzani wao tena wakipewa sapoti kubwa na mashabiki wao wenye vurugu na wanaoshangilia muda wote.

Al Ahly wanatumia Uwanja wa Cairo International unaoingiza mashabiki 75,000 lakini jambo kubwa uwanjani hapo ni kitendo cha mashabiki wanaongozwa na kikundi cha Ultras Ahlawy.

Post a Comment

0 Comments