Windows

KOCHA YANGA AWATANGULIZIA MAOMBI SIMBA


Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa anaomba Mungu ili timu ya Simba ifanikiwe kutwaa ubingwa wa Michuano ya SportPesa Cup.

Yanga iliondolewa juzi kwenye michuano hiyo baada ya kuchapwa na Kariobang Sharks kwa mabao 3-2, huku watani zao Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC leopards jana.

Baada ya Simba kushinda, sasa wanakuwa wameenda nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake anachota kitita cha dola 30,000.

“Sisi tumeondolewa, naomba sana Simba ambao waweze kutwaa ubingwa huu,” alisema Zahera raia wa Congo ambaye timu yake inaongoza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments