Uongozi wa klabu ya Yanga juzi ulianza kulipa madeni ya mishahara ya miezi miwili ya nyota wao
Hadi kufikia kesho Ijumaa, Disemba 13 2019 wachezaji wote watakuwa wamelipwa stahiki zao zote
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema mpaka kufikia kesho jioni, wachezaji wote watakuwa wamelipwa
"Kufikia kesho (13/12/2019) saa 10:00 Jioni tatizo la kutolipwa mishahara ya wachezaji Yanga SC litakuwa limekwisha," amesema
Juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alikiri wachezaji kudai malimbikizo ya mishahara ya miezi miwili na akaahidi kuanza kulipa mishahara hiyo mara moja
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments