Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema malimbikizo ya madeni ambayo uongozi mpya umeyakuta ni matokeo ya hali ngumu ya kiuchumi ambayo timu hiyo imepitia katika kipindi cha miaka miwili
Juzi Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alitaja suala la madeni kuwa chanzo cha timu hiyo kushindwa kumudu baadhi ya gharama
Hata hivyo Kaya amesema ni muhimu kwa viongozi kuweka kipaumbele kwa yale masuala muhimu ili kuhakikisha timu inasonga mbele
Pia amesema suluhu ya changamoto hizo ni Yanga kubadili mfumo wake wa uendeshaji
"Sasa hivi ni wakati wa Klabu ya Yanga kubadilika na kugeukia mfumo wa uwekezaji na hisa hapo tutafikia malengo yetu," amesema Kaaya.
"Uongozi uliopita uliacha madeni kwa sababu tulikuwa na hali mbaya sana kila mtu aliona hali halisi ilivyokuwa, lakini uongozi wa sasa unapaswa kutoa kipaumbele kwa yale mambo ya muhimu kwa sasa ili kusonga mbele"
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments