Disemba 25 ambayo ni sikukuu ya XMas, mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wao watakuwa uwanja wa Uhuru kuikabili Lipuli Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mabingwa hao wa nchi wanakabiliwa na michezo minne katika kipindi cha siku tisa
Baada ya mchezo wa Disemba 25, watashuka tena dimbani Disemba 28 kuikabili KMC kisha kufunga mwaka Disemba 31 kwa kuikabili Ndanda Fc
Ikumbukwe kabla ya michezo hiyo, wataanza na mchezo wa kombe la FA (ASFC) siku ya Jumapili Disemba 22 kwa kuikabili Arusha Fc
Mechi zote zitapigwa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam
0 Comments