Majeraha aliyopata mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula, yamepelekea kushonwa nyuzi kadhaa juu ya jicho lake la upande wa kushoto
Manula aliumia jana wakati akitekeleza majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Bara kwenye mchezo wa nusu fainali michuano ya Chalenji dhidi ya Uganda
Manula aliyekuwa nahodha wa Kili Stars alitolewa dakika chache kuelekea mapumziko baada ya kupata jeraha hilo
Kili Stars iliondoshwa mashindanoni baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0
Habari njema ni kuwa Manula ataweza kupona majeraha yake kwa wakati na pengine atakuwa tayari kuwakabili Yanga January 04 2020 kwenye mchezo wa ligi kuu
0 Comments