Mshambuliaji kinara wa mabao kikosi cha Simba Meddie Kagere amepewa ruhusa kwenda kwao Rwanda kumjulia hali mama yake ambaye ni mgonjwa
Mshambuliaji huyo atarejea kwa wakati kuuwahi mchezo wa raundi ya tatu kombe la FA dhidi ya Arusha Fc
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Disemba 22 kwenye uwanja wa Uhuru
Kagere ndiye kinara wa mabao kwenye ligi, akiwa na mabao nane
Mshambuliaji huyo raia wa Rwanda ni kama amezaliwa upya chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na kocha Sven Vanderbroeck anayesaidiwa na Selemani Matola
Kwani amekuwa na takwimu za kutisha za ufungaji kwenye mazoezi ya vinara hao wa ligi kuu ambayo yanafanyika katika uwanja wao wa Mo Simba Arena ulioko Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es salaaM
0 Comments