Mchezo wa kwanza wa benchi jipya la ufundi Simba ni dhidi ya Arusha Fc ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu kombe la Azam (ASFC)
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Disemba 22 kwenye uwanja wa Uhuru
Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema mchezo huo una umuhimu mkubwa kwao kwani ndio mchezo wao wa kwanza tangu watue Simba
Aidha Matola amesema wanahitaji kufuta rekodi mbaya ya Simba ya kutolewa katika raundi hiyo misimu miwili mtawalia
"Nafahamu mchezo dhidi ya Arusha Fc hautakuwa mwepesi kwani nao wanahitaji matokeo ili wasonge mbele raundi inayofuata," amesema
"Hivyo tunajiandaa kikamilifu ili tuweze kupata matokeo mazuri. Huu utakuwa mchezo wetu wa kwanza, tunahitaji ushindi ili tuwape furaha mashabiki wetu"
Ni wazi Arusha Fc watapaswa wajiandae 'kisaikolojia' kwani watakumbana na kikosi kamili cha mabingwa hao wa nchi
Katika misimu miwili iliyopita Simba haikuweka mkazo mkubwa katika michuano hiyo, lakini sio msimu huu
Simba imedhamiria kushinda kila taji ambalo timu hiyo itashiriki
Lakini zaidi ni kuwa kocha Sven Vanderbroeck hatakuwa tayari kuishuhudia timu yake ikikosa matokeo kwenye mchezo wake wa kwanza
Kwani huo hautakuwa mwanzo mzuri kwake
0 Comments