Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar imeitangaza Kamati ya kusimamia Mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) na tarehe ya kuanza Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Omar Hassan Omar ‘King’ mashindano hayo yanatarajiwa kuanza January 5, 2020 na kumalizika January 13, 2020 ambapo jumla ya timu 8 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo ambayo yatachezwa kwenye viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba na Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja.
Katika timu 8 zitakazo shiriki Mashindano hayo 4 kutoka Zanzibar ambazo ni Zimamoto, Chipukizi, Jamhuri na Mlandege na 4 kutoka Tanzania bara ambazo ni Simba, Mtibwa, Yanga na Mabingwa watetezi Azam.
Mashindano hayo yamepangwa makundi mawili kundi A na B ambapo Kundi A kuna timu za Yanga, Jamhuri, Mlandege na Azam huku kundi B kuna Simba, Mtibwa, Chipukizi na Zimamoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis Salim na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdulla Said.
Wajumbe wa Kamati ni Khamis Mussa Omar, Issa Mlingoti, Seif Kombo Pandu, Mohamed Ali Hilali (Tedy), Aiman Othman Duwe, Fatma Hamad Rajab, Salum Ubwa Ali Khalil, Juma Mmanga na Suleiman Pandu Kweleza.
0 Comments