Windows

Sadney, Balinya wametoa somo Yanga



Yanga inalazimika kuingia gharama kukisuka upya kikosi chake kwenye dirisha dogo baada ya usajili uliofanywa kwenye dirisha kubwa kwenye baadhi ya nafasi kutokidhi mahitaji

Yanga ilifanya kosa la kumuamini zaidi kocha Mwinyi Zahera kusajili wachezaji bila ya timu kujiridhisha na uwezo wao

Pengine Kamati ya ufundi ilipaswa kuundwa mapema ili kuwafuatiliwa wachezaji wote waliopendekezwa na Zahera kabla ya kuidhinisha wasajiliwe

Baada ya makosa hayo naamini kamati hiyo itafanya kazi yake vyema sasa

Mpaka sasa Yanga tayari imevunja mikataba ya washambuliaji wawili Sadney Urikhob na Juma Balinya ambao usajili wao uligharimu Mamilioni

Hivyo ni wazi umakini unapaswa kuongezwa kuhakikisha makosa hayajirudii kwa washambuliaji watakaosajiliwa kuziba nafasi zao

Aidha, orodha ya nyota wa kigeni ambao wataachwa baada ya kuitumikia Yanga kwa miezi sita itaongezeka kwani uongozi wa timu hiyo umepanga 'kuwakata' wachezaji ambao mchango wao ulikuwa chini ya asilimia 30

Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store

Post a Comment

0 Comments