Windows

Yanga kucheza mechi za viporo kabla ya kuikabili Simba



Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa January 04 kwenye uwanja wa Taifa

Kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, Yanga inatarajiwa kucheza mechi nne kabla ya kukabiliana na watani zao wa jadi

Wataanza na mchezo wa raundi ya tatu kombe la FA utakaopigwa kati ya Disemba 21/22 kwenye uwanja wa Uhuru

Baadae Yanga itaelekea mkoani Mbeya ambako Disemba 24 itaumana na Mbeya City uwanja wa Sokoine

Simu tatu baadae, Disemba 27 itarudi uwanja wa Sokoine kuikabili Tanzania Prisons

Baada ya michezo hiyo Yanga itarejea jijini Dar ambapo Disemba 30 itacheza na Biashara United





Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments