PAAAMBEEE shoga tumekutana tena kwenye kona yangu mimi shangingi mstaafu mwingine fotokopi, nasikia kuna watu wanajiita mashangingi wastaafu sifa yao kubwa kunywa pombe za watu na kuambulia kipigo mikovu kibao kama kibaka mzoefu, heee heeeiyaaaa! Shoga leo nimelikoka likakolea! Nimelivalia dera lazima niiname nilichekeze, upo? Vijana wa mjini wanakwambia bora upishane na mwendokasi siyo treni za umeme na ukitaka kujua tikiti ni maji au tunda kula na mbegu zake, halooo eeeeeh!
Siku zote tutashindana lakini mimi nitabakia namba moja, najua ujuayo na usiyojua, kaa chini mwali nikufunde ulikimbia unyago hujui mizungu inaokotwaje. Ndiyo maana nikasema mtashindana lakini hamtashinda namba moja nitabakia mwenyewe. Paaaambeeeee eeehhh!
Wapo wanaotaka eti tukutane hadharani tuoneshane nani zaidi, bado nakuelezeni msipoteze muda wenu kunijadili moja mpaka kumi nimekamata miye sijui ninyi wenzangu mmeshika namba ngapi hata kwenye kumi bora hampo.
Hebu nipishe niwape raha au unataka umaarufu kupitia jina langu, sikukatazi lakini kimoyomoyo unajua kabisa Anti Nasra namba moja yake mpaka kumi ila kuanzia kumi na moja kanyaganeni huko siwaingilii. Hebu tuzungumze kilichotutoa majumbani kwetu na kununua gazeti kisha kuisoma kona hii.
Leo nataka kuzungumza na mijanamume yenye kukimbilia kwa waganga kuongeza ukubwa wa nyeti. Jamani nakuulizeni ninyi waganga wa kienyeji mnaoongeza ukubwa wa bakora mnajua ukubwa wa chungu anachokwenda kuingiza mwiko wake?
Unajisikia raha gani unapoingiza mwiko kwenye chungu, mwenzio anauma meno kwa maumivu nani alikuambia raha upate wewe peke yako. Basi leo nataka kuwaelezea kitu kimoja hasa ninyi mnaojiona bakora zenu fupi.
Usikimbilie kwa mganga kuongeza ukubwa, nani aliyekuambia ukubwa wa mkono ukoleza utamu wa ngoma. Au udogo wa mkono hupunguza utamu wa ngoma? Hebu nisikilize tena nisikilize kwa makini kutomfurahisha mpenzio si udogo wa mwiko bali kujua kuutumia, unakimbilia kuongeza ukubwa wa nanihino ili umfurahishe mkeo au umkomoe?
Siku zote vita ni mbinu si manguvu mengi na mwenye nyumba kamwe hanyimwi chakula! Hilo wala hatulikatai lakini siyo basi ufanye kumkomoa mkeo. Hivi nitaongea hadi lini na mate yanikauka, jamani utamu wa mahaba uwe mtundu wa kujua nikae engo gani mpenzio anapokuwa amekaa mkao fulani. Wengi najua hamjui matumizi ya mitindo ya mapenzi (staili) maana ya mitindo ya mapenzi ni kutokana na maumbile ya mwanaume, upo nyonyo?
Kama mafupi mpenzio unatakiwa umuweke mtindo gani kama marefu vile vile mpenzio unatakiwa umuweke mtindo gani. Ukishajua matumizi ya staili za mapenzi hutasumbuka kukimbilia kwa waganga, hivi nani aliyekuambia mpaka ufike chini ya mchanga ndipo mpenzio apate raha, jamani raha zinapatikana hata mwanzo mwa kisima kwa kujua kuteka maji kwa kata.
Huchoti maji mengi jaza kidogo… kidogo… kidogo… kidogo, hebu kajaribu umsikie mpenzio atakupa salamu gani. Pia nataka kuwaeleza wote wanaokimbilia kuongeza ukubwa wa bakora zao, mnajua madhara yake?
Basi nataka kukueleza maumbile yaliyo bora ni yale uliyoumbiwa na Mungu, ukiyaongeza baada ya muda huishiwa nguvu na kujikuta kwenye tatizo lingine la kutafuta nguvu za kiume.
Waulize waliyoongeza ukubwa sasa hivi wanajuta ngoma ikilala hainyanyuki tena wamebakia kula kwa macho mikono kupapasa bila kufaidi. Bakora zao zimebakia kama magobore ya mbao hayana kazi bora wayakate wawashie moto wa kuchemshia maji.
Hebu jaribu kuchukulia hata mfano mdogo shoga, ulishaona wapi kucha zinazokuna kwa raha ni ndefu, siku zote kucha fupi zina raha zake, ukiwa na kucha ndefu huwezi kumkuna mtu zaidi ya kumuumiza na kumsababishia vidonda. Nina imani nimesomeka, basi ndiyo mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu
The post Mwenye nyumba hanyimwi chakula appeared first on Global Publishers.
0 Comments