Windows

 LEBO ZA KIMATAIFA… KIBA ANAKWAMA WAPI ?

MWAKA huu unaweza kuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ baada ya kufanikiwa kufanya kolabo na staa wa R&B kutoka Marekani, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ kupitia Ngoma ya Blow My Mind.

Katika ngoma hiyo, imeweka rekodi ya kuangaliwa mara milioni 11 ndani ya wiki tatu tu katika Mtandao wa Youtube. Lakini ukiachana na kolabo hiyo, Davido anashikilia rekodi ya kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 12 ambao ni wengi kuliko msanii yeyote nchini mwao.

Mkali huyu pia, alishafanya kolabo nyingi za kimataifa, kuna Fansi Mi aliomshirikisha rapa Meek Mill wa Marekani, Ngoma ya Swing alioshirikishwa na memba wa Migos, Quavo na nyingine kibao.

Ukiweka kando ngoma, Davido alishaweka rekodi ya kuusimamisha Ukumbi wa 02 Arena nchini Uingereza baada ya kuwajaza ‘wazungu’ 20,000 katika shoo yake. Ndiye anayeongoza kwa kufanya shoo nyingi na mastaa wa ‘dunia’, ameshapanda jukwaa moja na wakali kama 50 Cent, Eminem, Nicki Minaj, Cardi B, Meek Mill, Drake na wengine kibao.

Nyuma ya yote hayo, Davido yupo chini ya Lebo ya Sony Music Entertainment (SME) ambayo ndiyo inayomsimamia pia staa wa Bongo Fleva, Alikiba. Lebo hiyo ndiyo iliyompa mafanikio marehemu Michael Jackson, ndiyo inayowapa heshima mjini DJ Khaled, Beyonce, Shakira, Celine Dion, Mariah Carey, JLo, John Legend, Alicia Keys na wengine kibao.

KIBA KUNANI?

Mei, 2016 Alikiba alisaini lebo hiyohiyo akiwa ndani ya Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini. Licha ya kusaini kwa mbwembwe na matarajio yakiwa makubwa, Alikiba aliishia kufanyiwa video ya Aje akiwa chini ya lebo hiyo hadi leo kimya.

Kwa sasa zimebaki tetesi, ikiwemo ya kuunganishwa kufanya kolabo na staa wa kimataifa, Ne-Yo ambayo kolabo hiyo inadaiwa kusimamiwa na Sony na ameifanyia Nairobi, Kenya.

DIAMOND

Licha ya kumiliki lebo yake ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Diamond amesaini pia katika lebo ya kimataifa ya Universal Music Group.

Lebo hiyo inawasimamia wasanii wakubwa kibao kama Lady Gaga, Rihanna, Taylor Swift, Kanye West, Jay Z, Iggy Azalea, Adele na Nasty C kutoka Afrika Kusini.

Diamond ameonekana kufaidika kwa lebo hiyo kwani ameshafanya Ngoma ya Marry You aliomshirikisha Ne-Yo ambayo ilivunja mauzo ya nakala kwa kiwango cha Platnum mara sita mfululizo kwa mjumuisho wa mauzo kutoka kwenye maduka yanayouza nyimbo kama vile iTunes, Spotify, Deezer na mengineyo.

Pia mwaka huu kupitia lebo hiyo, amefanikiwa kufanya kolabo na mkali wa Muziki wa Dansi kutoka Congo DR, Fally Ipupa kupitia Ngoma ya Inama ambayo imetazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 20 ndani ya miezi miwili tu Youtube.

WIZKID

Mkali huyu kutoka Nigeria naye licha ya kuwa na lebo yake ya Starboy, anamilikiwa na lebo ya kimataifa ya RCA Records ya Marekani ambayo inawasimamia wakali kibao akiwemo Chris Brown, Pink, Christina Aguilera, Justin Timberlake, R Kelly, Usher Raymond, Backstreet Boys na wengine kibao.

Wizkid kupitia lebo hiyo imemsimamia kwenye Ngoma ya Sweet Love, Fever akiwa na Tiwa Savage ambayo imeshatazamwa na watu zaidi ya milioni 30 katika Mtandao wa Youtube.

Kupitia lebo hiyo, ameshapanda jukwaa moja na Chris Brown, Drake, Beyonce na wengine kibao.

CASSPER NYOVEST

Rapa huyu anayekimbiza kwa Muziki wa Hip Hop kutoka Afrika Kusini naye yupo chini ya Lebo ya Universal Music Group inayomsimamia Kiba na Davido.

Mkali huyo, mwaka jana alisaini lebo hiyo ambayo tayari mwanga wa kutoboa zaidi unajionesha baada ya kuachia Ngoma ya Sweet and Short yenye mahadhi ya Kwaito. Pia walimuwezesha kupanda steji moja na Jay Z na Beyonce

The post  LEBO ZA KIMATAIFA… KIBA ANAKWAMA WAPI ? appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments