

Wakati uongozi wa Yanga ukiwa bado haujaweka wazi hatma ya nafasi ya kocha mkuu baada ya kumtimua Mwinyi Zahera mapema mwezi huu, makocha 21 wameinoa timu hiyo tangu mwaka 2000
Kaimu Kocha Mkuu wa sasa Charles Mkwasa ni miongoni mwa makocha ambao wameshikilia nafasi hiyo kwa vipindi tofauti
Msimu wa mwaka 2001/02 Mkwasa alikuwa kocha Mkuu kabla ya kurejea tena kuwa kocha msaidizi wakati wa awamu ya pili ya Hans van Pluijm
Pamoja na uwingi wa makocha hao, ambao CV zao 'zimeshiba', Yanga imefanikiwa zaidi kwenye soka la ndani
Imekwama wapi 'kutusua' Kimataifa na ifanye nini iweze kufanikiwa?
Hebu tizama makocha waliopita Yanga katika kipindi cha miaka 20;
1. Raoul Shungu (DRC) 2000
2. Charles Boniface Mkwasa(Tz) 2001
3. Jack Chamangwana (Malawi) (rip) 2002-2004
4. Jean Polycarpe Bonganya (DRC) 2004
5. Syllersaid Mziray (Tz (rip) 2004
6. Kenny Mwaisabula (Tanzania) 2005
7. Jack Chamangwana (Malawi) (rip) 2006
8. Milutin Sredojevic ‘Micho’ (Serbia) 2007
9. Razack Ssiwa (Kenya) 2007
10. Jack Chamangwana (Malawi) (rip) 2007
11. Dusan Kondic (Serbia) 2008-2010
12. Kostadin Papic (Serbia) 2010
13. Sam Timbe (Uganda) 2011
14. Kostadin Papic (Serbia) 2011
15. Tom Saintfiet (Ubelgiji) 2012
16. Ernie Brandts (Uholanzi ) 2012-2013
17. Hans Van Pluijm (Uholanzi) 2013-2014
18. Marcio Maximo ( Brazil ) 2014
19. Hans Van Pluijm (Uholanzi ) 2015-2016
20. George Lwandamina (Zambia) 2016-2018
21. Mwinyi Zahera (DR Congo) 2018-2019
22. ????????
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjanj kutoka Play Store.



0 Comments