Windows

Nyota Simba wanogesha mazoezi Kilimanjaro Stars



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' leo kimeemdelea na mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kujiandaa na michuano ya CECAFA Chalenji inayofanyika kuanzia mwishoni mwa wiki nchini Uganda

Wachezaji saba wa Simba walijumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na kocha Juma Mgunda akishirikiana na Selemani Matola

Wote tayari wameripoti kambini na kushiriki kikamilifu mazoezi ya timu hiyo





Mlinda lango Aishi Manula anaongoza orodha ya nyota hao. Wengine ni Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Miraji Athumani

Kilimanjaro Stars inatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa Alhamisi kuelekea Uganda

Watacheza mchezo wa kwanza dhidi ya ndugu zao Zanzibar Heroes Jumapili, Disemba 08



Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments