Timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Uganda licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Sudan katika mchezo uliopigwa leo
Kili Stars imefuzu hatua hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kundi B ikijikusanyia alama nne nyuma ya vinara Harambee Stars ambao wameshinda mechi zote tatu ukiwemo mchezo uliopigwa mapema dhidi ya Zanzibar
Zanzibar Heroes ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kenya na hivyo kuondoshwa kwenye michuano hiyo
Kilimanjaro Stars huenda ikakutana na wenyeji Uganda Cranes kwenye mchezo wa nusu fainali
Kwa habari zaidi Download App ya Soka kiganjani kutoka Play Store.
0 Comments