Windows

UONGOZI YANGA WAKIRI KUSHINDWA KUFANYA BIASHARA YA JEZI


Yapo maswali mengi sana kuhusiana na namna au wapi zinapatikana jezi au tracksuit original zinazovaliwa na wachezaji wa @yangasc kwa ajili ya mashabiki (replica).

Ukweli ni kwamba msimu huu klabu haina replica yoyote ya kuuzwa kwa mashabiki, lakini imekuwa ikinunua au kupokea vifaa kutoka kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Hii imefanya timu kuwa na jezi na vifaa vingine vingi kuliko misimu mingine yote.! .
Hakuna shida ya vifaa klabuni kwa sasa ni kweli kabisa, lakini tatizo liko sehemu moja tu..! ‘kibiashara’.

Kupatikana kwa vifaa na kukosekana kwa replica kumekuwa kukitoa mwanya kwa ‘maharamia’ kulivamia soko na kuuza jezi na vifaa hivyo bila faida yoyote kwa klabu, miaka nenda miaka rudi.

Wakati mwingine ni vigumu kuwazuia watu wasiuze wakati wewe huna na bidhaa inahitajika sokoni.

Licha ya jitihada kubwa kufanyika kujaribu kuzuia uharamia,mara hii changamoto imekuwa kubwa zaidi hasa baada ya ‘kufeli’ kwa mambo tarajiwa yaliyokuwa ndani ya makubalino na kampuni ya vifaa ya macron.

Ni wazi kwamba kwa sasa klabu haina KIT SPONSOR / KIT MANUFACTURER na hapo ndiyo mwanzo au shina la klabu kutokupata faida yoyote kwenye uuzwaji wa jezi na vifaa vingine.

Baada ya uchunguzi na utafiti wa muda, msimu ujao klabu itakuja na mfumo mpya wa uuzaji wa vifaa vyake vyote.

Utaratibu utaanza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya huku wawakilishi (waliopata kibali) wakipewa nafasi ya kusimamia uuzwaji wa bidhaa mikoani, hivyo kufanya nchi nzima kuvipata vifaa kwa wakati mmoja.

Duka la klabu ambalo kwa miaka mingi limefungwa litakuwa la kwanza kufunguliwa na kutoa nafasi kwa maduka mengine maalumu kila mkoa yatakayokuwa yamepewa kibali kutangazwa na hatua kali kwa wasio na kibali kuchukuliwa.

Ununuzi online kupitia website ya klabu utakuwa umeunganishwa vizuri kuwawezesha watu wengine kufanya manunuzi popote duniani na mapato kuingia moja kwa moja klabuni.

Huu ndiyo wakati kwa wale wote ambao wangependa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kibiashara yaliyo salama na faida kwa klabu wawasialiane na uongozi kwa Maelekezo zaidi, kwa sababu ziko taratibu nzuri zililoandaliwa.

Matayarisho ya vifaa kwa ajili ya msimu mpya yameshaanza.

Na Dismas Ten

Post a Comment

0 Comments