

Ishu ya usajili wa kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata sio tetesi tena kwani kiungo huyo anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kusaini mkataba wa kuitumikia Simba, imefahamika
Taarifa za uhakika ni kwamba tayari kiungo huyo anayemaliza mkataba kuitumikia Gor Mahia ameshatumiwa tiketi ya Ndege ili aje kumalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Simba inataka kumsajili Kahata kabla hajaingia timu ya Taifa ya Kenya ambayo itasafiri nchini Ufaransa kwenda kuweka kambi kujiandaa na fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Misri mwezi ujao
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Simba amethibitisha Kahata kutumiwa tiketi ya Ndege akitarajiwa kuwasili nchini kabla ya Jumamosi
Jana Mtendaji wa Simba Crescentius Magori alisema wanafahamu Kahata anamaliza mkataba Gor Mahia na ameshaaaga timu hiyo kuwa hataongeza mkatabacut
Hata hivyo Magori hakuweza wazi kama Simba tayari imeanza mchakato wa kumsajili
Usajili wa Kahata unatajwa kuja kuimarisha zaidi safu ya kiungo katika ushambuliaji
Kwa sasa Simba inawategemea Clatous Chama, Haruna Niyonzima na Hassani Dilunga



0 Comments