

Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili anasubiri kujua hatma yake katika klabu ya Yanga huku akiwa na ofa kadhaa mkononi
Kabwili aliyemwishoni mwa mkataba wake, ana ofa kutoka nchi za Arabuni na Sudani
Hata hivyo mwenyewe amesema bado angependa kuitumikia Yanga hivyo kama hakutakuwa na makubaliano basi ataweka wazi wapi anaelekea
"Nina mazungumzo na timu kadhaa kutoka nje ya nchi. Mkataba wangu na Yanga unamalizika hivyo kila kitu kikikamilika nitaweka wazi," amesema
"Hata hivyo kipaumbele nimeipa timu yangu ya Yanga kwani bado niko hapa, nimelelewa vizuri na natamani kuendelea kubaki hapa"cut
Kabwili ni miongoni mwa wachezaji 18 ambao mikataba yao inamalizika hatma yao ikibaki mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera ambaye leo huenda akatangaza majina ya wachezaji ambao hawataongezewa mikataba mipya
Mbali na Kabwili, wachezaji wengine wanaomaliza mikataba Yanga ni pamoja na Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma, Matheo Anthony na Mrisho Ngasa
Wengine ni Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Ibrahim Ajib, Amissi Tambwe na Haruna Moshi



0 Comments