

Shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu zitakuwa mkoani Morogoro ambapo mabingwa wa msimu wa pili mfululizo, Simba watakabidhiwa kombe baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar
Mgeni rasmi katika hafla hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, ni Mh Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani
Mashabiki wa Simba mkoani Morogoro wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo itakayofanyika saa 11 jioni baada ya kumalizika mchezo unaotarajiwa kuanza saa tisa Alasiri
Uwanja wa Jamhuri leo utapendeza kwa rangi nyekundu na nyeupe kwani ukiacha mashabiki wa Simba wa mkoani Morogoro, wapo mashabiki kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na kutoka jijini Dar es salaam ambao tayari wako Morogoro
Huo ni ubingwa wa 20 kwa Simba
Aidha timu zote 20 zinatarajiwa kushuka dimbani leo kukamilisha msimu
Mechi zote zitapigwa muda mmoja (saa kumi) isipokuwa mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba ambao utaanza saa tisa Alasiri



0 Comments